Magufuli atoa tahadhari kwa vyombo vya habari

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo mbali mbali vya habari  kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.
  • "Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue,"  Dkt Magufuli aliyasema maneno haya wakati akiwaapisha Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.

  • "Kwa kuwa wewe ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."

  • "Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndiyo mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika," amesema Dkt Magufuli

Comments

Popular Posts