SHABIKI WA CHELSEA MWENYE ROHO NGUMU AMSHAMBULIA JOSE MOURINHO

“Tunapenda sana Jose Mourinho kuwa kocha wa Chelsea. Ni kocha mkubwa katika historia ya klabu yetu. Lakini sasa mashabiki wanaendelea kuchoshwa na tabia zake.
Haiwezi kupita siku asitokeze kwenye vichwa vya magazeti kwa habari mbaya.
Tumemaliza suala la kutosalimiana na Arsene Wenger, sasa yupo kwenye bifu mpya tena.
Maamuzi ya Mourinho kumshambulia daktari wetu ni ya kipumbavu. Kumuita daktari ni mjinga, yeye ndiye mjinga zaidi.
Kwanini suala hili lisingeongelewa chumbani?
Maana ya kumshambulia Carneiro hadharani ni nini?
Mwanamke huyo ni mtu maarufu mashabiki na wachezaji wa Chelsea. Kuendelea kurushiana maneno kuelekea mechi yetu kubwa dhidi ya Manchester City wikiendi hii inaleta picha mbaya zaidi.
Nikiwa shabiki wa Chelsea na Mourinho, naamini hii ni moja ya njia yake ya kucheza na akili za watu.
Hataki timu itokee kurasa za nyuma ya magazeti kwasababu ya matokeo mabaya, anahamisha akili za nyota wake kuelekea mechi ya Etihad.
Hili limeniudhi sana. Jose kwa mara nyingine amekosea sana ingawa haitokei mara zote

Comments

Popular Posts